The things hardest to bear are sweetest to remember. – Lucius Annaeus Seneca
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NGUMU KUBEBA, NZURI KUKUMBUKA…
Kwenye maisha yetu, huwa hatupendi mambo magumu,
Tunapenda mambo yawe rahisi na yasiyo na changamoto zozote.
Lakini kila tunapokaa na kukumbuka tulipotoka, huwa tunakumbuka yale magumu tuliyopitia na kuyavuka.
Huwa tunakumbuka namna tulivyokutana na changamotonau ugumu na kuweza kuuvuka.
Ni mara chache sana utafikiria mambo yaliyokuwa rahisi na kuyafurahia.
Hivyo rafiki, unapokutana na ugumu au changamoto, usijaribu kuzikimbia, badala yake zitatue na itakuwa kumbukumbu nzuri sana kwako kwa baadaye.
Yote magumu tuliyowahi kupitia, yametengeneza kumbukumb nzuri kwetu kama tuliyatatua.
Tatua ugumu wowoe unaopitia sasa ili uweze kujitengenezea kumbukumbu nzuri za baadaye na ujijengee sifa ya kuweza kupambana na magumu zaidi.
Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha