Tunahitaji kuwahamasisha watu kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yetu. Kwa kuwa kila tunachohitaji kwenye maisha yetu kinatoka kwa wengine, kadiri tunavyokuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine, ndivyo inavyokuwa rahisi kwetu kupata chochote tunachotaka.

Sisi binadamu tunaongozwa na hisia kuu mbili;

Moja ni tamaa ya kupata zaidi, kila mtu anapenda kupata zaidi ya kile ambacho anacho.

Mbili ni hofu ya kupoteza, hakuna anayependa kupoteza kile alichonacho.

Kwa hisia hizi mbili, tunapata njia mbili za kuwahamasisha watu;

Moja; kuwaonesha watu nini wanapata kwa kuchukua hatua fulani, hapa unatumia ile tamaa yao ya kupata zaidi.

Mbili; kuwaonesha watu nini wanapoteza wasipochukua hatua, hapa unatumia ile hofu yao ya kupoteza.

Furaha

Sasa katika njia hizi mbili, moja ina nguvu kubwa kuliko nyingine.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wanasukumwa zaidi na kukosa kuliko kupata. Yaani watu watahamasika zaidi kuchukua hatua kama kuna kitu wanakosa, kuliko wanavyohamasika kama kuna kitu watapata.

Kwa mfano kukiwa na uchaguzi wa kupata shilingi elfu kumi au kupoteza shilingi elfu kumi, watu watachukua hatua zaidi kuepuka kupoteza elfu kumi kuliko hatua wanazochukua ili kupata elfu kumi.

SOMA; UKURASA WA 726; Kilichojificha Nyuma Ya Hofu Ya Kufanya Mambo Makubwa….

Hivyo kwa lolote unalofanya, kama unataka watu wawe tayari kuchukua hatua zaidi, usiwaoneshe tu nini wanapata kwa kuchukua hatua, bali waoneshe pia kipi wanapoteza kama hawachukui hatua.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog