It is better, of course, to know useless things than to know nothing. – Lucius Annaeus Seneca
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Ni siku nyingine mpya, siku siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HAKUNA MAARIFA YAENDAYO BURE…
Kitu chochote unachojifunza kwenye maisha yako, kiwe kikubwa au kidogo, kiwe kibaya au kizuri, kuna siku utahitaji kukitumia kwenye maisha yako.
Hii ina maana kwamba, hakuna chochote unachojifunza ambacho unaweza kusema kimekupotezea muda.
Kuna wakati utakuwa umekwama mahali na kile ulichowahi kujifunza kikawa ukombozi kwako.
Hivyo rafiki yangu, jifunze sana, pata maarifa mbalimbali. Usidharau chochote unachojifunza kwa sababu hujui kitakuja kukufaa wapi. Na kwa hakika, lazima kitakufaa.
Na hata kama huna nafasi ya kujifuna mambo mkubwa na ya maana, jifunze hata mambo madogo na yasiyo na maana.
Ni bora kujifunza jambo la hovyo kuliko kutokujifunza kabisa.
Kwa sababu chochote unachijifunza kinatanua akili yako zaidi, kinakifanya uone vitu tofauti na ulivyozoea.
Lakini usipojifunza chochote, akili inasinyaa, inaendela na kile ilichozoea.
Jifunze leo, jifunze kila wakati na jifunze chochote unachoweza kupata cha kujifunza. Hakuna marifa yanayokwenda bure, ipo siku utapata nafasi ya kuyatumia.
Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha