“Where fear is, happiness is not” – Lucius Annaeus Seneca
Hongera rafiki yangu kwa siku hii bora sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HOFU NA FURAHA HAVIWEZI KUKAA PAMOJA…
Kama umewahi kusikia ule usemi kwamba fedha haiwezi kununua furaha, au watu wenye mali nyingi huwa hawana furaha, tatizo kubwa ni hofu.
Mara zote, hofu na furaha haviwezi kukaa pamoja.
Hivyo mtu anapokuwa na fedha nyingi halafu akawa anahofia kuzipoteza,
Au mtu akawa na mali nyingi lakini akawa na hofu ya kuzipoteza, hawezi kuwa na furaha.
Ukishakuwa na hofu juu ya kitu, furaha haiwezi kuwepo juu ya kitu hicho.
Na kama tunavyojua, hofu na furaha vyote ni vitu vinavyoanzia ndani ya mtu, hivyo ndani ya mtu haviwezi kukaa vyote pamoja.
Kama unataka kuwa na furaha juu ya kitu chochote, ondokana kwanza na hofu ulizonazo juu ya kitu hicho.
Usikubali hofu ikuzuie wewe kuwa na maisha ya furaha, mengi unayohofia wala hayatokei, lakini yanakunyima wewe furaha.
Ukawe na siku bora sana leo, isiyo na hofu na yenye furaha tele.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha