KITABU; Meditations / Marcus Aurelius.
UKURASA; 38 – 47.

Ni tabia yetu binadamu kutaka watu wawe kama tunavyotaka kuwa sisi.
Kutaka wafanye kile tunachotaka wafanye na hata kufikiri vile tunavyotaka sisi wafikiri.

Marcus anatuambia huku ni kupoteza muda wetu, kwa sababu hatuwezi kuwafanya wengine wawe kama tunavyotaka siai.
Wala hatupaswi kuwasema vibaya, wala kuwafikiria wanafikiria nini. Tuishi sisi kwa ubora na kuwaruhusu wengine nao waishi.

Kama kuna chochote ambacho tungependa wengine wajifunze au wawe, njia bora ya kuwashirikisha ni kukiishi. Kuwa na maisha bora yanayoendana na kile unachotaka wengine wakiige. Na hapo watakuwa na uhuru wao wenyewe wa kuchukua hatua au kubadilika.

Marcus anatukumbusha pia ya kwamba muda wetu ni mfupi sana, na muda pekee tulionao, ni muda tulionao sasa.
Kupoteza muda huu kwa jambo lolote ambalo siyo kubwa na la maana, ni kuchagua kupoteza maisha.

Kwa kuwa muda ni mfupi na wa thamani sana Marcus anatuambia;
Tusifanye jambo lolote ambalo hatukubali ndani ya mioyo yetu,
Tusifanye jambo lolote ambalo tutajutia kufanya.
Tusifanye jambo lolote kwa sababu ya sifa za nje.
Tuaifanye jambo lolote ili kutimiza tamaa zetu.

Badala yake, tujue yale muhimu kabisa kwetu na yenye mchango mkubwa kwa wengine na tutumie muda wetu kuyafanya.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha