Habari za leo rafiki?

Mwaka 2017 ndiyo unaelekea ukingoni na muda siyo mrefu tutauanza mwaka 2018. Wakati mwaka 2017 ulipoanza, watu wengi walisema na kupanga mengi kwa mwaka huu 2017. Lakini siku zilivyokuwa zinaenda, ndivyo wengi walivyosahau yale waliyopanga na kurudi kuishi kwa mazoea.

Hichi ni kitu ambacho kimekuwa kinawatesa watu wengi kwa miaka mingi, wanaweka malengo na mipango ile ile kila mwaka lakini hawawezi kuikamilisha. Kwa kipindi kirefu kila mwanzo wa mwaka nimekuwa nakuandalia semina kwa njia ya mtandao, semina ya kukupa uhalisia wa mwaka mzima na jinsi gani ya kukuendea.

Kusudi kubwa la mimi kuandaa semina hizi za mwanzo wa mwaka ni kuwasaidia watu waache kujidanganya na yale maneno ya mwaka mpya mambo mapya, au mwaka huu nitafanya hicho, kile na kile, wakati mtu wala hajabadili chochote kwenye maisha yake.

Nilichojifunza kupitia usomaji wa vitabu na uzoefu wangu binafsi na hata wa wengine ni kwamba hata upange mambo makubwa kiasi gani, kama hutaanza kubadilika wewe mwenyewe, hakuna chochote kitakachobadilika.

Na kwa hakika, kitu ambacho kimekuwa kinawaangusha wengine, ni kutaka mabadiliko ya nje wakati ndani bado hawajabadilika. Hivyo kusudi langu kubwa ni moja, mabadiliko yaanzie ndani yako, uanze kubadilika wewe kabla hujataka kubadili kitu kingine chochote.

Na kila mwaka, mwanzoni nimekuwa nakushirikisha namna bora ya kubadilika, jinsi ya kujenga mifumo mizuri ya maisha ambayo itakuwezesha kufanikiwa kila siku na kwa mwaka mzima.

Kwa mwaka huu mpya tunaouendea wa 2018, nimekuandalia semina ya siku 5 itakayoendesha kwa njia ya mtandao. Semina hii itaendeshwa kwenye mtandao wa WASAP ndani ya kundi la KISIMA CHA MAARIFA, kundi ambalo kwa mwaka mzima unaendelea kujifunza kila siku.

Mada za semina.

Kwenye semina hii ya kuuanza mwaka 2018, tutajifunza mambo yafuatayo;

Siku ya kwanza; karibu mwaka mpya, jitengeneze wewe kuwa mpya.

Siku ya pili; maneno matatu ya kutuongoza kwa mwaka 2018.

Siku ya tatu; mfumo bora wa siku na maisha ya mafanikio.

Siku ya nne; fedha na uwekezaji kwa mwaka 2018

Siku ya tano; hatua za kwenye kazi, biashara na mahusiano kwa mwaka 2018.

Kwa siku hizo tano tutajifunza kwa kina na kila mmoja wetu kuondoka na mpango wa kuishi na kufanyia kazi kwa mwaka 2018. Mpango ambao utazuia changamoto au matatizo kuwa kikwazo kwetu kupata kile tunachotaka.

Tarehe ya kufanyika kwa semina.

Semina itafanyika kwa siku tano, kuanzia jumatatu ya tarehe 08/01/2018 mpaka ijumaa ya tarehe 12/01/2018.

Jinsi ya kushiriki semina hii.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama, hakuna gharama za ziada za kulipa ili kushiriki semina.

Kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= (elfu hamsini). Hii ni ada ya mwaka mzima, kwa kipindi cha miezi 12 tangu unapojiunga.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaendelea kujifunza mengine mengi kila siku, ikiwa ni pamoja na kushiriki semina nyingine ya njia ya mtandao na semina ya kuhudhuria pia.

Jinsi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Unalipa ada tsh 50,000/= kwa njia ya simu; MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Namba hizo zina jina AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwenye moja ya namba hizo kisha utaunganishwa kwenye kundi la WASAP.

Mwisho wa kujiunga ili kushiriki semina.

Japokuwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni muda wowote mtu unaotaka, ili unufaike na semina hii, ni muhimu ujiunge kabla haijaanza, ili uweze kushiriki somo la kwanza mpaka la mwisho.

Hivyo tarehe ya mwisho ya kujiunga ili kushiriki semina hii itakuwa ijumaa ya tarehe 05/01/2018.

Karibu sana tuuanze na kuenda na mwaka 2018 kwa pamoja, tuweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO