When you arise in the morning, think of what a precious privilege it is to be alive – to breathe, to think, to enjoy, to love. – Marcus Aurelius

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa nafasi hii nzuri sana ya leo, nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NI UPENDELEO WEWE KUWA HAI LEO…
Unapoamka leo, fikiria ni upendeleo wa kiasi gani ulioupata wewe,
Nafasi hii nzuri sana ambayo wewe umeipata lakini wapo wengine ambao hawajaipata.
Kwa kugundua umuhimu na upendeleo uliopata, itakuwa jambo la ajabu sana kama utaanza kulalamika kwa lolote, au kuona kama maisha hayakufai.
Itakuwa ajabu zaidi kama utamua kupoteza muda huu wa kipekee uliopata, ambao kuna wengine walitamani sana waupate lakini haikiwezekana.

Thamini sana kila nafasi unayoipata, ichukulie kama fursa ya kipekee kwako kwenda kuishi kwa ubora zaidi.
Usilalamike, kulaumu au kupoteza muda huu wa kipekee kwa namna yoyote ile. Bali angalia njia bora za kuutumia ili kuweza kupiga hatua zaidi.

Nikutakie siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha