A happy life is one which is in accordance with its own nature. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii ya kipekee sana kwetu.
Siku bora sana ambapo tuna nafasi ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Kwa mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA mwaka huu 2018 unazidi kuwa mwaka wa kufanya makubwa.

Asubuhi hii tutafakari IJUE ASILI YA MAISHA YAKO…
Kila maisha yana asili yake na kila mtu ana asili yake.
Kuna vitu ambavyo kwa wengine ni rahisi kufanya ila kwako ni vigumu.
Na kuna vitu ambavyo kwako ni rahisi kufanya ila kwa wengine ni vigumu.

Kuna uwezo, vipaji na hata tabia za kipekee kwa kila mmoja wetu.
Lakini siyo wote wanajua kile halisi kilichopo ndani yao.
Kwa sababu wengi wanalazimishwa kuwa kama wengine, wakiamini ndiyo njia sahihi.

Lakini njia sahihi ni tofauti kwa kila mtu,
Na njia sahihi inatokana na asili ya mtu.
Na mtu anapoijua asili yake, akaijua njia sahihi kwake, inakuwa rahisi kwake kuweza kufanya makubwa.

Na hata maisha ya furaha ni zao pa mtu kujua na kuishi asili yake.
Maana asili ndiyo uhalisia, na ndiyo mtu anaweza kutumia vizuri kila kilichopo ndani yake.
Ijue asili yako, ishi kwa asili yako na utapata matokeo bora kabisa na furaha kubwa pia.

Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha