Kama kuna mambo makubwa ambayo unataka kufanya kwenye maisha yako, ambayo yanakutaka uchukue hatari kubwa, na hilo linakupa hofu, basi njia mbadala ni kuchukua hatari ndogo ndogo kwenye maisha yako.

Sisi binadamu ni viumbe wa mazoea, huwa tunafanya zaidi kile tulichozoea kufanya kuliko ambacho hatujazoea. Hivyo unapojifunza kuchukua hatari ndogo ndogo kwenye baadhi ya maeneo ya maisha yako, unajijengea uzoefu ambao unaweza kuutumia kwenye maeneo makubwa.

Biashara

Hivyo angalia maisha yako na ona ni hatari zipi ndogo ndogo unaweza kuchukua. Hatari ambazo hata ukishindwa au kupoteza haitakuumiza sana, kisha kazana ufanikiwe ili kujijengea uzoefu ambao utakupa kujiamini na kuweza kuchukua hatua kubwa zaidi.

SOMA; UKURASA WA 998; Kushinda Kwa Gharama Yoyote Ile…

Mfano mzuri sana ni kwenye biashara, kama unataka kuanza biashara kubwa lakini una hofu itashindwa, huku fedha unazopanga kutumia siyo zako, unaweza kuanza na biashara ndogo kabisa. kwa kuanza hivi, unajifunza na pia unajijengea kujiamini kwenye biashara.

Kitu chochote ambacho mtu unafanya kwa mara ya kwanza, huwa kunakuwa na ile hali ya kutokujiamini, na hii ndiyo inafanya hofu kuwa kubwa zaidi. Hivyo kama utaanza kwa hatua ndogo, zitakujenga kujiamini na hapo utashangaa unapata ujasiri wa kufanya makubwa zaidi.

Popote ulipokwama sasa hivi, chagua mahali unapoweza kuanzia kwa hatua ndogo sana, na hilo litakukwamua hapo ulipokwama.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog