Utu ni kufanya kile ambacho ni kizuri kwako na kwa wengine pia. Japo hili siyo jambo rahisi kufanya, hata kama inaonekana ni rahisi kiasi gani.
Ni kawaida kwa binadamu kupiga uzuri, kupinga kile ambacho mtu unajitoa kufanya kwa ubora wa hali ya juu.

Pamoja na kupingwa huko kwa uzuri, kuacha kufanya uzuri ni kuchagua kuharibu utu wako. Ni thamani kwako kupigania kufanya kwa uzuri, kufanya kwa ubora, kwa sababu huo ndiyo unakufanya wewe kuwa mtu.
Wakati mwingine utaona haina haja ya kufanya uzuri kama unazungukwa na watu wasiojali, unaona haina haja ya kuweka juhudi wakati kila mtu anafanya kawaida.
Unapofika kwenye hali kama hizi, kumbuka hili muhimu, hufanyi kwa ajili ya wengine, bali unafanya kwa ajili yako binafsi. Hivyo endelea kufanya uzuri, endelea kufanya kwa ubora kwa sababu ni wewe unanufaika na matokeo unayoyapata.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog