When we are well, we all have good advice for those who are ill. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nzuri na ya kipekee kwetu.
Ni nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kupata matokeo bora sana.
Kwa mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tutaweza kufanya makubwa mwaka huu 2018.

Asubuhi ya leo tutafakari UKIWA VIZURI UNAKUWA NA USHAURI MZURI…
Tuanze na maswali muhimu,
Ni yupi ambaye utachukua kwake ushauri wa kuwa na afya njema, mtu ambaye kila wakati ana maradhi mbalimbali au yule ambaye afya yake ni imara?

Hata kama mtu ana ushauri mzuri kiasi gani, kama maisha yake binafsi yako kinyume na ushauri huo, inakuwa vigumu sana kwetu kusikiliza ushauri huo.
Maana tutajiuliza kama ushauri huo unafanya kazi, mbona yeye hajautumia?

Hivyo kama tunataka watu wachukie ushauri wetu,
Kama tunataka watu watuangalie kama mfano,
Kama tunataka kuwa alama nzuri kwa wengine,
Basi tunapaswa kuishi kile ambacho tunawaambia wengine,
Tunapaswa kuwa tayari tunakiishi na kinatuletea matokeo bora.

Usikazane na ushauri kama unachosema ni tofauti kabisa na unachoishi, hakuna atakayekusikiloza na kukuamini.
Na hili ni kwenye maeneo yote ya maisha yetu.
Ukawe na siku bora sana leo, kuwa vizuri ili uweze kutoa ushauri mzuri.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha