Everything that exists is in a manner the seed of that which will be. – Marcus Aurelius

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ni mwongozo wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2018.

Asubuhi ya leo tutafakari ULIVYO LEO NI MBEGU YA KESHO…
Kitakachotokea kesho kwenye maisha yako siyo muujiza,
Bali kitakuwa ni zao la zile hatua ambazo umechukua leo.
Kinachotokea leo kwenye maisha yako siyo bahati mbaya au nzuri, bali ni mbegu uliyoipanda siku za nyuma.
Kila kitu ambacho kinatokea kwenye maisha yetu, tunakuwa tumekitengeneza sisi wenyewe, tumekipanda kwa yale tunayofanya au tunayoacha kufanya.

Changamoto kubwa ni kwamba watu huwa wanapenda kubadili matokeo badala ya kubadili kinachozalisha matokeo.
Ni sawa na kupanda mbegu ya limao lakini wewe unataka machungwa. Hivyo mche unapotoa malimao, unajiambia uyachume malimao yote na kuyaondoa, ili baadaye yatoke machungwa.
Je inafanya kazi hiyo?

Jinsi ambavyo ktu upo leo.
Kile unachofikiria leo,
Hatua unazochukua leo,
Ndiyo mbegu inayozalisha kesho yako.
Hivyo kama unaitaka kesho bora, hakikisha unaanza kuwa bora leo, kwa kuchukua hatua ambazo ni bora kabisa.

Ukawe na siku bora sana ya leo mwanamafanikio.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha