“You are essentially who you create yourself to be and all that occurs in your life is the result of your own making.” – Stephen Richards

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo mwanamafanikio.
Ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuishi kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA na kuweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ni UUMBAJI WAKO MWENYEWE…
Maisha unayoishi sasa, umeyatengeneza wewe mwenyewe,
Kila hali ambayo unapitia kwenye maisha yako, umeitengeneza wewe mwenyewe.
Hivyo kama kuna kitu kwenye maisha yako hukifurahii, basi jua ya kwamba ulikitengeneza mwenyewe na ni wajibu wako kukibadili.

Hata kama mambo yanaonekana magumu kiasi gani, bado wewe mwenyewe una mchango mkubwa wa pale maisha yako yalipo sasa.
Ulichofanya siku za nyuma ndiyo kimekufikisha hapo ulipo sasa.
Utakachofanya leo ndiyo kitatengeneza kesho yako.
Unachofanya au unachoacha kufanya ndiyo kinachangia unakofika kimaisha.

Swali muhimu sana kujiuliza kabla hujafanya chochote ni je hichi ninachofanya, kinachangiaje kuyafanya maisha yangu kuwa bora zaidi?
Kama unaingia kwenye mitandaonya kijamii kila mara, kutaka tu kujua nani kafanya nini, jiulize je hilo linachangiaje maisha yako kuwa bora zaidi?
Kama unatumia saa nzima kila siku kufuatilia habari, jiulize je hilo linachangiaje kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi?

Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kwenye maisha yako,
Kila kitu unakiumba wewe mwenyewe, kwa kufanya au kutokufanya baadhi ya mambo.
Nenda kafanye uumbaji bora wa maisha yako leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha