“Take the course opposite to custom and you will almost always do well.” -Jean-Jacques Rousseau
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2018.
Asubuhi ya leo tutafakari KINYUME NA MAZOEA…
Vitu vyote vizuri huwa vinafanyika kinyume na mazoea…
Mafanikio yote makubwa huwa yanapatikana kinyume na mazoea..
Na tofauti kati ya watu huwa ni zao la kinyume na mazoea.
Watu wanapata kile ambacho wamekuwa wanapata wakati wote kwa kuwa wanafanya kwa mazoea.
Na kama wanataka kupata tofauti, hatua ya kwanza ni kwenda kinyume na mazoea.
Mazoea ni sumu, mazoea ni kaburi la mafanikio na mazoea ni kikwazo cha maisha ya furaha.
Chochote unachokwenda kufanya kwenye maisha yako, jikumbushe kufanya kinyume na mazoea.
Angalia umekuwa unafanyaje wakati wote, kisha jiulize unawezaje kufanya tofauti na ulivyozoea.
Ukawe na siku bora sana leo, siku ya kufanya kinyume na mazoea.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha