Every individual has a place to fill in the world and is important, in some respect, whether he chooses to be so or not. —Nathaniel Hawthorne
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2018.
Asubuhi ya leo tutafakari UMEIJAZA NAFASI YAKO HAPA DUNIANI?
Kila mmoja wetu anayo nafasi ya kujaza hapa duniani.
Kipo kitu ambacho ni wewe pekee unayeweza kukifanya kwa namna fulani hapa duniani.
Kila mmoja wetu anao umuhimu mkubwa sana hapa duniani.
Kuna kitu ambacho ukikifanya unaifanya dunia kuwa sehemu bora sana ya kuishi.
Swali ni je unaijaza nafasi yako hapa duniani?
Je kipo kitu cha tofauti kabisa unachofanya ambacho hakuna mwingine anafanya?
Kuijaza nafasi yako hapa duniani, kunahitaji ujasiri wa hali ya juu.
Kwa sababu ni rahisi kuiga kile wengine wanafanya kuliko kufanya chako mwenyewe.
Lakini hakuna anayefanikiwa kwa kuiga.
Hivyo wewe kama mwanamafanikio, chunguza maisha yako, jitathmini na ona kama unaishi utofauti wako au unafuata mkumbo.
Kama hujaanza kuishi utofauti wako hujachelewa, unaweza kuanza sasa.
Ijaze nafasi yako hapa duniani.
Ipe dunia kile umekuja hapa kuipa.
Usiidhulumu dunia.
Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha