You have power over your mind – not outside events. Realize this, and you will find strength – Marcus Aurelius
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NGUVU ZAKO ZILIPO…
Huna nguvu ya kuweza kuipanga dunia iendeje,
Mambo yatatokea kwa namna ambavyo yanatokea, iwe unapenda yanavyotokea au la.
Hivyo nguvu yako haipo kwenye yale yanayotokea, bali nguvu zako zipo ndani yako, kwenye fikra na mtazamo wako.
Huwezi kubadili yale yanayotokea na kufanya yatokee kama unavyotaka, ila unaweza kubadili fikra na mtazamo wako juu ya yale yanayotokea.
Kwa kuona uzuri na manufaa ya chochote kinachotokea, hata kama kwa wengine kinaonekana ni kibaya.
Hakuna kitu chochote ambacho kinatokea kwenye maisha yako kisiwe na manufaa kwako.
Labda kitakusaidia kusonga mbele zaidi, au kitakufanya uwe imara zaidi.
Tumia nguvu zako vizuri, kazana na kilicho ndani yako, badili kilicho ndani yako na acha kujisumbua na yale ya nje.
Huwezi kuipanga dunia kama unavyotaka mwenyewe, ila unaweza kujipanga na kuikabili dunia namna unavyotaka mwenyewe.
Kujua hili ndiyo uhuru wa kweli,
Kujua hili ndiyo hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye mafanikio.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia vizuri nguvu zilizopo ndani yako.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha