Habari za leo rafiki yangu?

Twiga ni mnyama mrefu kuliko wote duniani, na urefu wake unamwezesha kula majani yaliyopo kwenye kilele cha mti wowote. Hili linamfanya aweze kuishi kwenye mazingira magumu ambayo wanyama wengine hawawezi kuyaishi.

Simba ni mnyama mkali na mwenye mbio sana, kitu ambacho kinamwezesha kuwawinda wanyama wengine na akapata chakula. Bila ya ukali na mbio zake kali, simba hawezi kupata chakula kwa urahisi na atakufa.

Kwa asili, kila kiumbe hai ametengenezwa kwa namna ambavyo ataweza kuishi kwenye mazingira yake, samaki wa baharini, ambapo maji ni ya chumvi, wana chumvi kwenye miili yao kuliko samaki wa kwenye ziwa ambapo maji siyo ya chumvi.

Lakini katika viumbe wote waliopo duniani, yupo kiumbe mmoja ambaye anaonekana hana sifa na nguvu walizopewa viumbe wengine, lakini anaweza kuwatawala wote.

Kiumbe huyo ni binadamu. Sisi binadamu hatuna zile sifa ambazo wanyama wengine wanazo, sifa zinazowatofautisha na wengine, lakini kwa namna fulani tunaweza kuwatawala na kuwatumia wanyama wote.

Na hii ni kwa sababu tuna kitu kimoja ambacho wanyama na viumbe wengine hawana. Sisi binadamu tuna utashi, tunao uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi, na hii ndiyo nguvu yetu kwenye asili, hichi ndiyo kinatufanya kuweza kuitawala dunia na viumbe wengine waliopo hapa duniani.

Lakini sasa, kila mtu kuwa na utashi, na kila mtu kuwa na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi haimaanishi kila mtu anatumia uwezo huo vizuri.

Ndiyo maana hata baina ya watu, kwenye mazingira yale yale, wapo ambao wanafanya vizuri na wapo ambao hawafanyi vizuri. Kwenye kazi au biashara moja, kuna watu wanafanikiwa sana na wengine wapo tu wanasukuma siku.

Matumizi mazuri ya uwezo wetu wa kufikiri na kufanya maamuzi, ndiyo unaoleta tofauti kwenye maisha yetu na ya wengine.

Sasa swali linakuja, kwenye maisha yako yote, ni wapi umewahi kufundishwa kuhusu kufikiri? Wapi umewahi kupata darasa kuhusu kufikiri na kutumia uwezo wako wa ndani vizuri?

Tafakari kwa kina na utaona hakuna, hata shuleni ambapo ulitegemewa ujifunze mengi, umefundishwa historia za miaka mingi iliyopita, na ukazikariri ili ufaulu mtihani, lakini hukufundishwa kufikiri na kutafakari kwa kina.

Ipo njia moja bora ya kuwafanya watu wafikiri kwa kina na kuweza kutumia vizuri uwezo wao wa kufanya maamuzi. Njia hiyo ni kupitia falsafa.

Falsafa? Neno gumu tena hapo. Huenda ukisikia falsafa unapata picha ya maprofesa wa vyuo vikuu, ambao wanatumia muda mwingi kujadili mambo, kubishana na kuoneshana nani anajua, halafu mwisho wa siku hakuna hatua zozote wanazochukua.

Hii ndiyo taswira ambayo falsafa zimebeba kutoka kwa watu, lakini siyo taswira sahihi.

Falsafa ni namna tunavyoyaishi maisha yetu, kwa hekima na busara. Falsafa inamaanisha kupenda hekima, hivyo mtu unapochagua kuishi kwa falsafa, maana yake unachagua kuishi ka hekima.

Je kuna maisha bora zaidi ya yale ya kuishi kwa hekima?

Zipo falsafa nyingi sana kwenye maisha, na iwe unajua au hujui, kuna falsafa ambayo unaiishi. Na katika zama hizi za utandawazi na mitandao ya kijamii, watu wanaishi kila aina ya falsafa, ambazo hata hawazijui.

Sasa kwa kuwa kila mtu anaishi falsafa, na kwa kuwa maisha hayawezekani bila ya falsafa, kipi bora, kuishi falsafa ambayo hata hujui ni falsafa au kuchagua kuishi falsafa ambayo itafanya maisha yako kuwa bora?

Kama unachagua kuishi falsafa ambayo itayafanya maisha yako kuwa bora, basi ipo falsafa moja yenye sifa hiyo, ambayo ni falsafa ya ustoa au kama inavyojulikana kwa kiingereza STOICISM.

ustoa

Ustoa ni falsafa ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 2300 iliyopita, ikiwa imedumu kuliko falsafa nyingi ambazo watu wanaamini na kuziishi sasa.

Ustoa haijawahi kuwa falsafa ya maonesho, ile ya kubishana kwamba kipi ni sahihi na kipi siyo sahihi. Bali ustoa mara zote imekuwa ni falsafa ya maisha, falsafa ya kujua kipi sahihi kufanya na kipi siyo sahihi.

Ustoa ni falsafa ya vitendo, ndiyo maana hata kama umesoma falsafa shuleni au chuoni, utakuwa umesikia falsafa na wanafalsafa wengi, lakini huenda hujawahi kusikia falsafa ya ustoa.

Hii ni falsafa bora sana ya kuishi, ni falsafa ambayo inakuondoa kwenye matatizo ambayo wengi wanakutana nayo, falsafa inayokuwezesha kuielewa dunia, na falsafa inayokupa misingi sahihi ya kuishi ambayo inakuwezesha kuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

Ustoa ni falsafa ya watu wote, falsafa isiyo na ubaguzi, falsafa isiyo na maigizo na falsafa ya kuchukua hatua.

Mara zote nimekuwa nawashauri watu kitu kimoja inapokuja kwenye ushauri wa maisha bora, chagua falsafa ya kuishi na ishi falsafa hiyo. Na kwa wale ambao wanapenda kuwa na maisha bora, maisha ya kutokuyumbishwa na dunia, maisha ya kujijua wao wenyewe na kuweza kujitumia vizuri, basi falsafa ya ustoa ndiyo sahihi kwa maisha yao.

Yapo mambo mengi ya kujifunza kuhusu falsafa ya ustoa na jinsi tunavyoweza kuitumia kupiga hatua kwenye maisha yetu. Na ili tuweze kuelewana vizuri, nimeandaa darasa maalumu kuhusu falsafa ya ustoa.

Darasa hili litafanyika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambapo tutapata nafasi ya kuijua falsafa hii vizuri na jinsi tunavyoweza kuitumia kwenye zama tunazoishi.

Kitu muhimu sana ninachotaka kukuambia rafiki, kuna kipindi falsafa hii ya ustoa ilipotea kabisa, watu hawakuwa wakiona umuhimu wake, lakini siku za karibuni falsafa hii imerudi kwa kasi, na hii inatokana na changamoto za maisha ya sasa, ambazo falsafa nyingi zimeshindwa kutatua. Ni falsafa ya ustoa pekee inayoweza kutatua matatizo na changamoto tunazopitia zama hizi, hivyo jifunze falsafa hii na anza kuiishi mara moja.

Karibu kwenye darasa la wiki ambapo wiki hii tutajifunza kuhusu falsafa ya ustoa.

Darasa litafanyika tarehe; 28/04/2018 (JUMAMOSI), MUDA; SAA 12 JIONI MPAKA SAA 2 USIKU.

Katika darasa hili la falsafa hii muhimu sana ya ustoa tutajifunza yafuatayo;

  1. HISTORIA FUPI YA FALSAFA YA USTOA NA WANAFALSAFA WANNE WALIOIKUZA FALSAFA HII.
  2. MISINGI MIKUU MINNE AMBAYO FALSAFA YA USTOA INASIMAMIA.
  3. MFUMO WA MAISHA KWA WANAFALSAFA WA USTOA, AMBAO UNAKUANDAA KUKABILIANA NA MAGUMU YA MAISHA.
  4. JINSI UNAVYOWEZA KUITUMIA FALSAFA YA USTOA KWENYE MAISHA YA KILA SIKU.
  5. MJADALA, SHUHUDA, MASWALI NA MAJIBU.

Chagua kuwa mwanafalsafa wa ustoa na utakuwa umechagua kuwa na maisha bora. Uzuri ni kwamba huhitaji kuwa na sifa zozote au kuomba popote kuwa mwanafalsafa wa falsafa hii bora kabisa. bali unachohitaji ni kuijua falsafa hii, kisha kuanza kuiishi mara moja na kuanza kufaidi matunda yake.

Hatua ya kwanza ya kuijua falsafa hii ni kushiriki darasa la wiki hii, ili kujifunza na kujua falsafa hii kwa kina.

Ili uweze kushiriki darasa hili, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kama bado hujawa mwanachama na hujui KISIMA CHA MAARIFA ni nini basi soma hapa kwa ufupi;

KARIBU UJIUNGE NA KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni blog maalumu ya mafunzo na hamasa kwa ajili ya kufikia mafanikio makubwa. Blogu hii inaambatana na kundi maalumu la wasap ambapo unapata mafunzo mbalimbali kila siku kwa kuwa ndani ya kundi hilo.

Hivyo unapojiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kusoma makala kwenye blog, makala za maisha, mafanikio, biashara, uwekezaji, falsafa na kadhalika. Makala hizi huwezi kuzipata sehemu yoyote ile duniani ila tu kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Ndani ya kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, kila siku utaianza na TAFAKARI yenye funzo na hamasa kubwa ya kukusukuma siku hiyo kuchukua hatua. Kila jioni utajifunza kupitia wengine na yale waliyojifunza. Kila wiki utapata nafasi ya kushiriki darasa linalohusu maisha na mafanikio. Pia kila mwaka kuna semina mbili zinazoendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia kundi la wasap na semina moja ya kukutana ana kwa ana.

Pia kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kila mwezi unapata maswali ya kujifanyia tathmini yatakayokufanya uone pale ulipo sasa, kule ulikotoka na hata unapokwenda. Maswali haya yatakufanya uone wapi unakosea na wapi unapatia, pia hatua zipi za kuchukua ili uweze kufika pale unapotaka kufika.

Yote hayo unayapata kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, ambapo unalipa ada ya shilingi 50,000/= (elfu 50 pekee). Hiyo ni ada ya mwaka, ambapo ukilipa utalipa tena baada ya mwaka kuisha tangu ulipolipa. Ukishalipa ada hiyo unapata mafunzo yote hayo bila ya gharama za ziada, isipokuwa tu semina ya kukutana ana kwa ana ndiyo unalipia malipo ya ziada.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, lipa ada, tsh 50,000/= kwa namba zifuatazo; MPESA – 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY – 0717 396 253, majina kwenye namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu pamoja na email kwa ujumbe wa wasap kwenda namba 0717396253 kisha utaunganishwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kama upo hapa duniani, na upo makini na maisha na mafanikio yako, basi kuna sehemu moja ambayo unapaswa kuwa, nayo ni KISIMA CHA MAARIFA. Ninakuambia hili nikimaanisha, kwa sababu najua ukiwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, hutabaki hapo ulipo sasa, nakuhakikishia hilo, lazima utajikuta unasonga mbele zaidi, hata kama unaona umekwama kiasi gani.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu sana tuwe pamoja, tujifunze na kuhamasika kila siku, na kuweza kuyafikia mafanikio ambayo ni haki yetu ya kuzaliwa.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Usomaji