Iwapo timu mbili zitaingia uwanjani, moja ikaenda kwa lengo la kushindwa na nyingine ikaenda kwa lengo la kutokushindwa, timu yenye nafasi kubwa ya kushinda ni ile inayoenda na lengo la kushinda.

Hata kwa wanaoangalia mchezo huo, watakaoburudika zaidi ni wale wanaoangalia mchezo wa timu inayokwenda kwa lengo la kushinda, na siyo inayoenda na lengo la kutokushindwa.

Taaluma

Kwenye maisha, unaweza kuwa na malengo ya kufanikiwa na kupata kile unachotaka, au ukawa na malengo ya kutokupoteza. Wanaofanikiwa kwenye maisha ni wale wenye malengo ya kupata huku wale wenye malengo ya kutokupoteza, wakipoteza zaidi na zaidi.

Ndani yako kuna nguvu kuu mbili, nguvu ya kwanza ni ile ya kuthubutu, ya kujaribu vitu vipya na vikubwa. Nguvu ya pili ni ile ya kujilinda, ya kuepuka kupoteza. Kila mmoja wetu ana nguvu hizi mbili na mara zote huwa zinashindana.

SOMA; UKURASA WA 1052; Anza, Mbele Kutakuwa Rahisi Zaidi…

Ndiyo maana kila unapofikiria kufanya kitu fulani, huenda utaona mafanikio yake, au utaona hatari yake, na mara nyingi vyote kwa pamoja, vikikuvuta kila upande.

Sasa upande unaoshinda, ni ule upande unaoulisha.

Kama unalisha upande wa kuchukua hatua, upande wa kujaribu, kwa kuona namna matokeo mazuri yatakuwezesha kupiga hatua, na hata kama ukishindwa utakuwa umejifunza, hilo litakupa hamasa na kujiamini kuchukua hatua.

Kama utalisha ile hofu ya kushindwa, na kuona kila nafasi ya kukosa na kuanguka, utatawaliwa na hofu na hutaweza kuchukua hatua kabisa.

Lisha nguvu sahihi itakayokusukuma kupiga hatua zaidi. Kwa sababu ile nguvu unayolisha, ndiyo inayokutawala na kuleta matokeo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog