“Intelligent individuals learn from every thing and every one; average people, from their experiences. The stupid already have all the answers.” — Socrates

Hongera mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa nzuri na ya kipekee kwetu, kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIWE MPUMBAVU…
Kama una majibi yote,
Kama tayari unajua kila kitu,
Kama hakuna kipya unachoweza kujifunza,
Basi jibu rahisi kwako ni hili, wewe ni mpumbavu.

Werevu hujifunza kwa kila mtu na kwa kila kitu, hujua kwamba kipo kitu cha kujifunza kwa mtu yeyote wanayekutana naye na chochote wanachoona.
Watu wa kawaida hujifunza kutokana na uzoefu wao wenyewe, kupitia makosa yao wenyewe.
Tatizo kubwa kabisa lipo kwa wapumbavu, ambao hawajifunzi chochote, kwa sababu wanaamini tayari wanajua kila kitu.

Wapumbavu ndiyo utawakuta wakilalamika pale kitu kinapotokea, badala ya kujiuliza wamekisababishaje na wanajifunza nini. Wanaamini siyo makosa yao, hawajifunzi, baadaye kitu hicho kinatokea tena.

Huwezi kufanikiwa kwenye maisha kama utakuwa mpumbavu.
Huwezi kuwa huru kwenye maisha kama utakuwa mpumbavu.
Ushauri rahisi na muhimu, na kitu cha kujikumbusha kila mara ni hichi, USIWE MPUMBAVU.
Jifunze kwa kila mtu na kwenye kila kitu. Kila wakati wa maisha yako uchukulie kama darasa, maana maisha yenyewe ni darasa.

Ukawe na siku njema sana leo.
#UsiweMpumbavu
#NUK-TAO
#SkinInTheGame
#WhateverItTakes
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha