Tunaishi kipindi cha kipekee, kipindi bora kabisa kuwahi kutokea duniani.

Kipindi ambacho, mtu anaweza kujifunza chochote, bila ya kuwa na kitu au mtu wa kumzuia.

Maarifa na taarifa ni nyingi na zinapatikana kwa urahisi, kwa yeyote anayezitaka.

Lakini pamoja na wingi huu wa taarifa na urahisi wa kupatikana kwake, ni wachache sana ambao wanaweza kuzitumia vizuri kuyafanya maisha yao kuwa bora.

Muda tulionao

Yaani pamoja na wingi wa maarifa, na urahisi wa kuyapata, hichi ndiyo kipindi ambacho watu wengi sana wanateseka kwa kukosa maarifa.

Unaweza kuona ni jambo la kushangaza, lakini huo ndiyo uhalisia. Ni sawa na mtu kufa kwa kiu wakati amezungukwa na chemchem inayotoa maji masafi na salama muda wote wa siku.

SOMA; UKURASA WA 968; Kitu Pekee Ambacho Huwezi Kufundishwa Na Yeyote…

Sehemu ya hili imekuwa inasababishwa na kelele za dunia, pamoja na wingi wa maarifa, kelele nazo zimekuwa nyingi. Hivyo watu wamekuwa wakipotezwa na kelele, wakiamini ni maarifa, kumbe siyo.

Kwa mfano mtu anapokazana kufuatilia kila habari inayoendelea, akiamini hapitwi na kila kinachoendelea, atapata habari kweli, lakini habari hazina maarifa ya kumwezesha mtu kupiga hatua kwenye maisha yake.

Mtu anajijaza kelele akiamini ni maarifa, lakini kelele hizo hazimsaidii.

Changamoto nyingine ni kwamba kelele hizo zinavutia kiasi cha mtu kuona ananufaika, wakati anajinyima fursa kubwa ya kupiga hatua.

Achana na kelele za dunia rafiki, weka juhudi zako kwenye kupata maarifa bora, na ukishayapata, yafanyie kazi, usikubali yawe ni ya kujifurahisha tu.

Kwa maana hiyo basi, chochote unachojifunza ambacho huwezi kutumia kwenye maisha yako ni kelele kwako, ni upotevu wa muda wako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog