“Even after a bad harvest there must be sowing” – Lucius Annaeus Seneca

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari BAADA YA MVUNO MABAYA…
Kila mkulima anajua kwamba, baada ya mvumo mabaya, kinachofuata ni kupanda.
Mkulima haachi kupanda msimu unapoanza kwa sababu alipata mavuno mabaya.
Badala yake anachagua mbegu bora na kujiandaa vizuri kwa msimu mpya.

Kadhalika kwenye safari yetu ya mafanikio,
Baada ya kushindwa kwenye kitu kimoja, unapaswa kuendelea na kingine kilichopo kwenye mipango yako.
Usiache kabisa safari ya mafanikio, kwa sababu umeshindwa kwenye kitu kimoja, au umeshindwa mara moja au hata mara 10.

Kushindwa siyo kigezo cha kuacha, bali kusindwa ni hatua unayopitia kabla hujashindwa.
Hivyo usiache kitu kwa sababu umeshindwa, kama ndiyo kile hasa unachotaka, ushindi utakuja baada ya kupitia hatua za kushindwa.

Endelea kuweka juhudi kubwa,
Endelea kuiangalia ndoto yako kubwa,
Endelea kuwa na matumaini,
Endelea kupiga hatua zaidi hata kama umeshindwa.

Mkulima haachi kupanda kwa mavuno yalikuwa mabovu, na wewe usiache kupiga hatua zaidi kwa sababu umeshindwa au kukwama.
Pambana mpaka upate kile unachotaka.

Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha