“Begin – to begin is half the work, let half still remain; again begin this, and thou wilt have finished” – Marcus Aurelius
Ni siku nyingine nzuri, siku mpya na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUANZA NI NUSU YA KAZI…
Kupanga ni rahisi, kusema ni rahisi, lakini kutekeleza kile ambacho mtu anapanga ndipo ugumu ulipo.
Kuanza kufanya chochote ambacho mtu umepanga kufanya, ni nusu ya kazi nzima ya kufanya.
Hii ni kwa sababu inahitajika nguvu kubwa kuanza kuliko kuendelea.
Ni sheria ya asili kwamba chombo kilichotulia kitaendelea kutulia pale kilipo, na chombo kilochopo kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo.
Unapoanza, unatumia nguvu kubwa kushinda ile nguvu ya kutulia, nguvu ya kutokufanya.
Ukishaanza, unahitaji nguvu kidogo kuendelea kufanya, kwa sababu mwendo unachochea mwendo zaidi.
Chochote unachojiambia utafanya, lakini unaahirisha, anza sasa kufanya.
Utakapoanza kufanya, utagundua kwamba mengi uliyokuwa unayaogopa wala siyo mabaya na magumu kama ulivyokuwa unafikiria.
Kuanza ni nusu ya kazi, anza sasa.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuanza chochote ambacho umekuwa unasema utafanya.
#OneLife #AllIn #DayOne #SkinInTheGame #WhateverItTakes
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha