“Man was born free, and he is everywhere in chains.” -Jean-Jacques Rousseau
Mwanamafanikio, hii ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ULIZALIWA HURU, KWA NINI UNAJIFUNGA?
Binadamu ndiye kiumbe pekee ambaye anazaliwa akiwa huru kabisa, lakini anatafuta njia ya kujiweka kwenye kifungo.
Na kinaweza kuwa kifungo chake mwenyewe au kifungo cha wengine.
Na kinachowafanya wengi kuingia kwenye kifungo ni hofu na kukosa nidhamu.
Hofu walizonazo watu zinatumiwa kuwaweka kwenye vifungo,
Na ukosefu wa nidhamu wa watu, unawafanya wawe chini ya watu wengine wanaoweza kuwawajibisha.
Pale unapojiambia kwamba huwezi kuishi bila ya kitu au mtu fulani jua upo kwenye kifungo.
Pale unapokuwa na hofu inayokufanya ushindwe kuchukua hatua fulani unakubali kuwa kwenye kifungo.
Pale mtu mwingine anapoweza kufanya maamuzi yatakayoathiri maisha yako upo kwenye kifungo.
Na pale mtu mwingine anapokuwekea wewe ukomo wa chochote ambacho hakipaswi kuwa na ukomo kwako, upo kwenye kifungo.
Bila ya kisahau, pale unaposhindwa kujisimamia mwenyewe kufanya unachotaka, mpaka usimamiwe na wengine, upo kwenye kifungo.
Ni wakati sasa wa kuamka na kuchukua uhuru wako, uhuru mkubwa uliozaliwa nao lakini umeupoteza kwa kuingia kwenye vifungo mbalimbali.
Hakuna yeyote atakayekupa uhuru huu, bali ni wewe mwenyewe unapaswa kuuchukua kama unautaka uhuru wako.
Na kama hutautaka, wengine watafurahia sana kukuweka kwenye vifungo vyao.
Ukawe na siki bora sana ya leo, siku ya kuchukua uhuru wako na kuishi maisha yako.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha