“The most powerful weapon on earth is the human soul on fire.” —Marshal Ferdinand Foch

AMKA mwanamafanikio,
Siku nyingine, siku mpya na ya kipekee kwetu imeshaingia kwenye mikono yetu.
Ni maamuzi yetu tunatumiaje muda tulionao kwenye siku hii bora na ya kipekee sana kwetu.
Tunaweza kutumia muda huu kufanya makubwa na kupiga hatua, au tunaweza kuupoteza kwa kuhangaika na mambo ya hovyo. Uchaguzi ni wetu.

Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, na mwongozo wetu kwa mwaka huu 2018 ni TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SILAHA HATARI SANA DUNIANI…
Silaha hatari zaidi duniani siyo risasi wala mabomu, siyo silaha za nyuklia au kemikali za sumu. Zote hizo ni hatari, lakini hazifikii uhatari wa silaha hii; NAFSI INAYOWAKA MOTO…

NAFSI INAYOWAKA MOTO ni silaha hatari sana duniani, ni silaha yenye nguvu kubwa sana, ambayo kamwe huwa haishindwi, hata mambo yawe magumu kiasi gani.
NAFSI INAYOWAKA MOTO ni silaha isiyoweza kuzuiwa na chochote, labda ule moto wa ndani uzime wenyewe.

Hivyo rafiki, kwa chochote unachotaka, iwashe nafsi yako moto, na hakuna kitakachoweza kuzuia nafsi hiyo.

HIVI NDIVYO UNAVYOIWASHA NAFSI YAKO MOTO
👉🏼Jua kwa hakika nini unataka na maisha yako, jua kwa kila hatua.
👉🏼Ona kwenye akili yako kwamba tayari unacho kile unachotaka, jione ndani ya vile unataka kuwa, ukiw na kila unachotaka.
👉🏼Weka mpango madhubuti wa kufikia kile unachotaka, unaoeleza kila utakalofanya kipata unachotaka.
👉🏼Jitoe maisha yako yote kuweka juhudi kuendea kile unachotaka, usiruhusu usumbufu mwingine wowote uchukie muda na nguvu zako, weka kila ulichonacho kwenye kile unachotaka.
👉🏼Kuwa kiziwi kwa wanaokuambia huwezi, wanaokukatisha tamaa, usiwasikilize hata na sekunde na chochot wanachokuambia usiwaelewe. Kuwa kipofu kwa yale ambayo wengine wanafanya kw maonesho, usijisumbue kufanya chochote ili kuonekana.
👉🏼Kila mara jifunze, kila wakati jifunze kitu kipya usichojua na kitumie kupiga hatua zaidi.
👉🏼Ukikutana na changamoto, na utakutana nazo nyingi, furahi, zikaribishe vizuri na jua ni sehemu ya wewe kukua zaidi.
👉🏼 PATA UNACHOTAKA AU FIA NYIANI UKIKITAFUTA

Uwe na siki bora sana ya leo, siki ya kuwasha na kuchochea zaidi moto unaowaka ndani yako.

#OnFire, #SkinInTheGame, #AllIn, #WhateverItTakes, #10X, #DayOne, #OwnTheDay,

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha