“There is only one way to happiness and that is to cease worrying about things which are beyond the power of our will” — Epictetus

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari VITU AMBAVYO VIPO NJE YA UWEZO WAKO…
Vitu vyote ambavyo vinatokea kwenye maisha yako, tunaweza kuvigawa kwenye makundi matatu.
Kwanza kuna vile ambavyo vipo ndani ya uwezo wako,
Na kuna ambavyo vipo nje ya uwezo wako.
Kwa vile ambavyo vipo ndani ya uwezo wao, kuna ambavyo unaweza kufanya kitu kuvibadili, na vingine huwezi kuvibadili.

Sasa, unapokutana na chochote kwenye maisha yako, swali la kwanza unapaswa kujiuliza je kipo ndani ya uwezo wako au nje ya uwezo wako?
Hilo ni swali la kwanza na muhimu, ambalo litakuongoza kwenye hatua unazokwenda kuchukua.

Kama kitu kipo ndani ya uwezo wako basi huna haja ya kuhofia, chukua hatua.
Na kama kitu kipo nje ya uwezo wako pia huna haja ya kuhofia, bali endelea na mambo yako.
Hakuna kiwango cha hofu kinachoweza kubadili chochote kwenye kitu kilichopo nje ya uwezo wako.

Epictetus, mwanafalsafa wa ustoa alituambia njia ya uhakika ya furaha ni kuacha kuhofia vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako.
Na ukiangalia kwa undani, sehemu kubwa ya vile tunavyohofia kwenye maisha yetu, vipo njenya uwezo wetu.
Tunajinyima furaha na pia tunajipotezea muda wetu na nguvu zetu kwa vitu ambavyo havitabadilika kwa namna yoyote.

Uwe na siki bora sana ya leo rafiki, siku ya kuchukua hatua kwa yaliyo ndani ya uwezo wako, na kuachana na yale yaliyo nje ya uwezo wako.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha