“If we encounter a man of rare intellect, we should ask him what books he reads.” — Ralph Waldo Emerson

Siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri kwetu sisi wanamafanikio kwenda kuchukua hatua kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MUULIZE ANASOMA VITABU GANI…
Ukikutana na mtu ambaye anajua vitu vya tofauti,
Mtu ambaye anajua vitu usivyojijua wewe, vitu muhimu kwa maisha ya mafanikio.
Ukikutana na mtu ambaye amepiga hatus kubwa kwenye maisha yake, ana mafanikio makubwa kuliko wengine.
Usimwonee wivu,
Usianze kusema huyu ana bahati,
Usitafute sababu kwamba alifanya namna fulani kufika pale alipo.
Bali omba kujifunza kwake, na kitu muhimu kabisa kumuuliza ni je anasoma vitabu gani, au anajifunza kwa watu gani.

Tunapozaliwa akili zetu zinakuwa kama daftari jipya, ambalo halina chochote kilichoandikwa.
Kadiri tunavyokwenda ndiyo tunajifunza.
Hivyo yeyote unayemwona leo anajua usichojua wewe, amejifunza, na hakushushiwa ujuzi huo ndotoni.

Hivyo ili na wewe ujue, ili na wewe upate maarifa bora waliyonayo wengine, kuwa tayari kujifunza.
Kuwa tayari kujifunza kwa kila mtu na kila hali.
Na hapo utaweza kujua mengi, na ukiyafanyia kazi utapiga hatua kubwa sana.

Kila wanachojua wengine wwmejifunza, hivyo na wewe pia unaweza kujifunza na kuwa bora zaidi.

Ukawe na siki bora sana leo, siku ya kujifunza na kuchukua hatua kubwa ili kuweza kufanikiwa.
Kumbuka kanuni yetu ya KISIMA CHA MAARIFA na nenda kaiishi leo; MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA.

#PataMaarifaSahihi #ChukuaHatuaKubwa #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #NiLeoTu #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha