Hongera mwanamafanikio kwa siku hii mpya na bora sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari WATU WA KUWAEPUKA KAMA UKOMA…
Watu wote kwenye maisha yako hawalingani,
Kuna watu ambao ukikutana nao unapata hamasa, ukienda kwa na wazo fulani unaondoka ukiwa na wazo liloloboreshwa zaidi na kuongezewa zaidi. Watu ambao ukiwa nao karibu hakuna kinachoshindikana, uwepo wa tu kwenye maisha yako wanakuwa kama moto unaokuchochea. Yaani kwa kuwaona tu, hata kama hawajaongea chochote, unapata hamasa kubwa.

Kwa upande wa pili kuna watu kwenye maisha yako ambao ukikutana nao unakata tamaa ya maisha. Ni watu ambao ukienda kwa na wazo jipya unaondoka huna wazo kabisa, unaondoka ukiwa umeshawishika kwamba ulichokuwa unawaza ni ujinga na haiwezekani kabisa.
Watu ambao ukiwa nao jaribu unajisikia tu kuchoka na huwezi kupiga hatua yoyote kubwa. Watu ambao kila ukiwa nao wanahubiri jinsi mambo ni mabaya na jinsi hali inazidi kuwa ngumu. Yaani ukiwaona tu watu hao, ukiwa nao karibu, hata kama hawajaongea, umeshaishiwa nguvu kabisa na huna tena hamasa ya kufanya makubwa.

Rafiki yangu, leo hii tafakari kila mtu unayekutana naye kwenye maisha yako, kila mwandishi unayemsoma, kumsikiliza au kumwangalia, kila kipindi unachofuatilia, na kila mtandao wa kijamii unaojihusisha nao.
Na angalia je watu na vitu hivyo vinaingia kundi lipi, kama ni kundi la kukupa hamasam endelea nao, kama ni kundi la kukukatisha tamaa, basi ogopa kama ukoma.

Na kumbuka, huhitaji kumwonea mtu huruma au kuanza kufikiria atakuchukuliaje kama mtu huyo ameingia kwenye kundi la wakatishaji tamaa, mkate haraka kama utakayokata magugu kwenye shamba lako la mazao muhimu.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kusafisha magugu kwenye maisha yako.
#Fanya #EpukaWatuHasi #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa #WhatEverItTakes

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha