Mpendwa rafiki,

Kama kungekuwa na vidonge vinauzwa dukani kama vile panadol vinavyosaidia watu kuwa na nidhamu basi ingesaidia kweli. Kwa bahati mbaya sana hakuna duka lolote linalouza dawa ya nidhamu binafsi, ukiwa na nidhamu binafsi tayari wewe umeshaweza kujitawala, unaweza kujiambia hapana hata kama una hamu au tamaa ya kitu fulani, huwezi kuusikiliza mwili hata siku moja, unaundesha mwili badala ya mwili kukuendesha wewe.

Maisha Hayajawahi

Ukiwa na nidhamu binafsi basi hisia za mwili haziwezi kukuendesha hata siku moja, utakua uziambia hapana mara moja na zinakutii.

Huwa tunajidanganya sana  katika maisha yetu na muda mwingine tunakuja kujilaumu kwa kujiambia laiti ningelijua bora hata ningelifanya hivi au vile. Huwa tunapata majuto mengi kwa sababu ya kutofanya kile tulichopanga kwa wakati husika. Kuna maneno mawili ambayo huwa yanatuungiza gharama sana katika maisha yetu. maneno hayo kama tukiyaondoa katika midomo yetu tutapunguza hatari nyingi za kujiakungusha kila mara.

Maneno nitafanya baadaye na nitafanye kesho yamekuwa ni njia nzuri sana ya kujidanganya na kujifariji. Ila ni maneno ambayo yamekuwa mwiba sana kwetu, yanatufanya tuwe na viporo vya kazi vingi na tukijiambia kesho au baadaye nitapata muda huo ni uongo kabisa wala hatutakuja kuupata bali tunajidanganya sisi wenyewe tu kuwa tutafanya lakini muda ukifika hatuwezi tena kufanya.

SOMA; Ufahamu Ugaidi Hatari Kuliko Wote Duniani Unaosumbua Maisha Ya Watu Wengi

Kama unakitu chako cha kufanya tafadhali kifanye sasa kama ulivyopanga usiloge kabisa kwa kujiambia baadaye au kesho. Ondoka haraka katika nadharia hiyo kesho au baadaye itakuja kukusababishia majuto makubwa sana na huenda mpaka sasa ukikumbuka mambo mengi uliyopoteza na kujiharibi ni mengi sana hivyo baadaye na kesho huwa inadhulumu ndoto za watu wengi sana.

Kesho haijawahi kuja wala baadaye yenyewe, ukifikia mahali unaona unataka kujiambia kesho au baadaye usikubali kuahirisha bali kataa sema hapana mpaka nimalize kile nilichopanga ni ujinga kuahirisha jambo nililopanga kufanya mimi mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo,  kataa maneno haya mawili yanayokudanganya hovyo kila siku ambayo ni nitafanya baadaye au kesho.

Hivyo basi, yote haya yanawezekana kama ukiwa na nidhamu binafsi katika maisha yako, na nidhamu binafsi huwezi kununua dukani hata siku moja hata utaweza kulipa watu wakusimamie kama ukishindwa kujitawala ni kazi bure.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !