“No one is going to hand me success. I must go out and get it myself. That’s why I’m here. To dominate. To conquer. Both the world and myself.” —Unknow

Siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NENDA KATAWALE…
Hakuna kitu chochote ambacho kinakuja kirahisi kwenye maisha yetu, hasa vitu vyenye thamani.
Kadiri kitu kinavyokuwa na thamani kubwa, ndivyo tunavyohitaji kuweka juhudi kubwa zaidi ili kuweza kukipata.

Unahitaji kwenda kutawala chochote unachofanya,
Kwenda kuangusha kila aina ya kikwazo kitakachosimama mbele yako,
Ndiyo uweze kupata kile unachotaka kupata.
Haitakuwa rahisi, lakini itawezekana.

Usiishie tu kusema unataka mafanikio,
Jikumbushe mafanikio hayatakufuata hapo ulipo wewe,
Bali mafanikio yanapaswa kusakwa, kupiganiwa, kuangushwa na kisha kitawaliwa.

Jukumu lako leo na kila siku mpya unayoianza, ni kwenda kitafuta, kuangusha na kutawala ili uweze kufanikiwa.
Kadiri unavyofanya hilo kwa uzuri kila siku, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu,
#Fanya #Tawala #Angusha #Pambana #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha