Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari AMINI KWENYE KILE UNACHOFANYA…
Rafiki, chochote ambacho unachagua kufanya na muda wako, inabidi iwe ndiyo kitu muhimu sana kwako kufanya na unahitaji kukiamini sana.
Unahitaji kuamini kwamba ndiyo kitu sahihi kwako kufanya.
Na unahitaji kuamini kwamba ndiyo kitu sahihi kabisa kwa wale unaowalenga.
Bila ya kuamini kwenye kile unachofanya, hutakifanya kwa moyo mmoja, hutaweka nguvu na juhudi kubwa kwenye kitu hicho.
Na bila kuamini unachofanya, hutaweza kuwashawishi wengine waamini na kuchukua hatua.
Hutaweza kuwashawishi wengine wanunue au kulipia kitu hicho kama huamini ndiyo kitu pekee sahihi kwao.
Imani uliyonayo kwenye chochote unachofanya, ndiyo itakayotengeneza mafanikio makubwa kwako.
Hivyo kama huamini kile unachofanya, ni bora hata usifanye, maana hakitakuwa na manufaa yoyote kwako na kwa wale unaowalenga.
Ukawe na siki bora sana leo, siku ya kujenga imani kubwa kwenye kile unachofanya.
#Fanya #ImaniHujenga #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha