Mpendwa rafiki,

Watu wengi wanaogopa kufanya, watu wachache ndiyo wanaweza kufanya je wewe uko katika kundi gani? watu hofu imewatawala tokea wanaamka mpaka wanaporudi tena kitandani,wanaishi maisha ili mradi siku iende tu. Ukiwa na hofu huwezi kufanya kitu chochote cha maana, kwanza hata ukweli huwezi kusema lakini pia hutoweza kutoa thamani yako yote kama mtu ambaye anajua kitu fulani.

Kwa wale ambao ni wakristu neno usiogope limeandikwa mara 365 maana yake kwamba kila siku unapoamka kutoka kitandani unatakiwa usiogope, unaamka na kwenda kuitawala siku yako mara moja bila kuogopa na unakwenda kuthubutu kufanya yale unayopenda, unafanya bila kuogopa chochote kwa sababu kuogopa ni hofu unayoijaza wewe mwenyewe katika akili yako.

BIASHARA NDANI YA AJIRA, HARD

Rafiki, kwanini watu wengi wanaogopa kuanza kufanya biashara? Watu wengi wanaogopa kuanza kufanya biashara kwa sababu biashara ni hatari, biashara ni changamoto. Hakuna kitu kirahisi hapa duniani, hata kukaa tu na kuweka mikono mifukoni ni kazi kwa sababu kama wewe uliyezoa kufanya halafu ukaambiwa ukaye bila kufanya itakuwa ni adhabu kubwa kwako.

Watu wengi wanaogopa hatari na sehemu ambayo ina hatari ni kwenye biashara wala hilo halina ubishi. Ni sehemu ambayo utaweza kujipatia kipato kile unachotaka lakini hatari hazikosekani. Watu wengi wanaogopa hatari ndiyo maana wanaogopa hata kuanza kufanya biashara. Unapofanya biashara lazima utakuna na changamoto hilo halina ubishi.

SOMA; Sababu Hizi Saba Ndiyo Zinakuzuia Kupata Mafanikio Makubwa Licha Ya Wewe Kuwa Na Juhudi Kubwa Kwenye Kazi Zako.

Kwenye biashara ndiyo shule yenyewe utaweza kujifunza kila kitu na kawaida ya watu wengi hawapendi shida ndiyo maana wanaogopa kuingia kwenye biashara kwa sababu wanajua biashara ni changamoto na ni hatari hivyo anaona sehemu pekee ya kuwa salama ni kutofanya biashara.

Rafiki, kama unataka kufanikiwa usiogope hatari wala changamoto, ingia katika mapambano ili mshindi aweze kupatikana, hakuna mashindano bila mshindi hivyo usitegemee kupata kombe lolote kama hujaingia uwanjani. Na wale ambao hawaogopi hatari ndiyo wanafanikiwa siku zote.

Hatua ya kuchukua leo, kama ulikuwa unaogopa kuanza biashara kwa sababu ya hofu basi ivunje hofu na jiambie kuwa hatari na changamoto ni kitu cha kawaida katika biashara. Ni kama usiku na mchana, macheo na usiku wewe ingia uanze kufanya na kuwa tayari kukabiliana na chohote.

Kwahiyo, kama unaendelea kuogopa hebu jiulize, utaendelea kubaki na kuogopa mpaka lini huku ukiendelea kuteseka? Si bora uingie kufanya lakini unajua unapata kipato chako kuliko kukaa  bila kuchukua hatua.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !