Siku mpya,
Siku bora,
Na siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KWA SABABU KILA MTU ANAONA…
Kuna wakati watu hufanya mambo ya hovyo kwa sababu wanaamini hakuna mtu anayeona.
Watu wanapokuwa mbele ya wengine, wanakuwa makini na yale wanayofanya kwa sababu wanajua kila mtu anaona.
Lakini wanapokuwa wenyewe, wqnaweza kufanya mambo ya hovyo sana wakiamini hakuna anayeona.

Unapaswa kufanya kila unachofanya kama vile kila mtu anaona.
Kwa sababu ni kweli kwamba kila mtu anaona, hata kama unafanyia kwenye giza nene kabisa na umejihakikishia hakuna anayeona.

Kwa sababu wewe unaona, na unajua unachofanya siyo sahihi, siyo unachotaka uonekane unafanya.
Hivyo nafsi yako itaendelea kukusuta wakati wote na kila anayekuangalia anajua kuna kitu unafanya ambacho siyo sahihi.

Jua unachotaka na jua unachopaswa kufanya ili kukipata.
Kisha nguvu zako na muda wako wekeza kwenye kupata unachotaka.
Achana na yale yasiyo muhimu na makini.

Na kwa kila unachojishawishi kufanua, fikiria kwamba kila mtu anakuangalia, fikiria televisheni ya taifa inaonesha live na kila mtu anashuhudia. Na jiulize kama ni kitu cha kishujaa ambachp utajivunia kuwa umekifanya.

Usijidanganye kufanya chochote cha hovyo ukiamini hakuna anayeona. Kila mtu anaona, huwezi kuihadaa dunia na huwezi kujidanganya wewe mwenyewe.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kifanya yale makini na kufanya kama vile kila mtu anaona, kwa sababu ni kweli kila mtu anaona.

#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #MudaNiSasa #WhatEverItTakes#WachaManenoWekaKazi

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha