Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIWEKEE UKOMO…
Moja ya vitu vinavyokuzuia usiweze kufanya mambo yako kwa wakati ni kwa sababu unakuwa huna ukomo.
Fikiria unapokuwa na kazi ambayo unapaswa kuikamilisha ndani ya wiki moja,
Siki tatu za mwanzo hutafanya kazi yoyote kubwa, utaona bado siku zipo.
Siku ya nne utaanza kujipanga vizuri ili ufanye kwa uhakika zaidi.
Siku ya tano utaanza kifanya kwa kiasi, lakini utajiambia una siku mbili.
Siku ya sita ndiyo utafanya hasa,
Na ile siku ya saba, siku ya mwisho, hutafanua chochote kile bali kazi ile ambayo ndiyo siku ya mwisho.
Hii ina maana kwamba, kazi ya siku saba, imefanywa ndaninya siku mbili.
Lakini imechukua siku saba kwa sababu mtu hukujiwekea ukomo, au ukomo ulikuwa mbali sana.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako, jiwekee ukomo, tena wa karibu.
Anza leo kwa kujiwekea ukomo wa kufanya kazi yako kwa nusu ya muda uliozoea kufanya.
Na kuhakikisha hujidanganyi kwenye hilo, weka mpango mwingine muhimu zaidi baada ya mida huo uliopanga kumaliza kazi yako.
Unapojiwekea ukomo, hasa wa muda na fedha unazohitaji kutumia kwenye kitu fulani, akilo yako inabidi ifanye kazi zaidi na uweze kuwa na njia bora zaidi ya kufanya.
Lakini kama utachukulia muda au fedha ni kitu cha kutumia tu kama kinavyopatikana, hutaweza kupiga hatua kubwa.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kujiwekea ukomo ilo uweze kufanya bila ya kupoteza muda au fedha.
#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha