Mafanikio yako kwenye maisha yanakwenda kwa kiwango unavyowapenda wengine.

Kadiri unavyowapenda wengi zaidi, ndivyo unavyoweza kufanikiwa zaidi.

Kwa saba bu chochote unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kutoka kwa wengine.

Na unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka.

Ni lazima uwapende sana watu kiasi cha kuyaachia maisha yako kwao, kuyatoa maisha yako kwa ajili yao.

Unapaswa kuwapenda watu kiasi kwamba kazi yako kubwa ni kuangalia wanawezaje kunufaika zaidi, wanawezaje kupiga hatua zaidi.

Unahitaji kuwapenda watu kiasi kwamba utakwenda hatua ya ziada katika kuwaandalia nafasi nzuri kwao kufanikiwa. Kwenye chochote unachofanya, unaweka mbele zaidi maslahi ya wengine, ukijali wanapata nini na wewe utapata unachotaka.

SOMA; UKURASA WA 943; Usiendeshwe Na Hofu Kwenye Maamuzi Haya…

Unapaswa kuwapenda watu kiasi kwamba unafurahi na kushangilia pale unapoona wamefanikiwa, na hata kama wamefanikiwa kukupita wewe. kwa sababu unajua kufanikiwa kwao ni kufanikiwa kwako, na kama wamefanikiwa wao, basi hata wewe utafanikiwa.

Wapende watu na mara zote kazana kukwepa na kumaliza misuguano na wengine. Boresha mahusiano yako na kila unayekutana naye kiasi kwamba mtu anaona ana wajibu wa kufanya kitu kwa ajili yako.

Ni kwa kiwango hichi ndiyo unakuwa umetengeneza nafasi nzuri kwako kufanikiwa.

Ni lazima uwapende sana watu kama unataka kufanikiwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha