Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UNACHAGUA MAUMIVU YAPI?
Kwenye maisha kuna maumivu ya aina mbili.
Yapo maumivu ya kufanya, pale unapofanya kile ambacho hukuzoea kufanya na kuhitajika kuweka juhudi zaidi ya ulivyozoea kuweka.
Na pia kuna maumivu ya kutokufanya, pale ambapo huchukui hatua halafu unabaki na majuto na hali ya kufikiria ninge…
Kila mtu anao uhuru wa kuchagua maumivu gani anayotaka kwenye maisha yake.
Lakini hakuna anayekwepa kabisa maumivu haya.
Wale wanaojaribu kukwepa maumivu ya kufanya wanaweza kufikiri kwamba wao ni wajanja na wameyashinda maumivu, ni mpaka pale wanapokuja kujikuta kwenye majuto, wakati ambao hawawezi kuchukua hatua yoyote ndiyo wanaumia zaidi kuliko hata wangefanya.
Usitake kusogeza maumivu mbele,
Usijaribu kuyakwepa maumivu.
Chagua maumivu gani upo tajari kuyavumilia na yakabili.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuyakabili maumivu ya kufanya na kutokujaribu kukwepa maumivu hayo.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha