“A man travels the world over in search of what he needs and returns home to find it.” — George Moore

Siku mpya,
Siki bora
Na siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye yale tuliyochagua kufanya, ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.

Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUTAFUTA AMBACHO TAYARI UNACHO…
Mara nyingi watu wamekuwa wanakimbizana na maisha, wakihangaika sana kutafuta kitu ambacho tayari wanacho.

Wanaenda mbali kabisa kutafuta kitu ambacho tayari kipo ndani yao wenyewe.
Karibu kila unachotaka kwenye maisha yako, chochote kile unachohitaji kupata au kufikia, tayari kipo ndani yako.
Hata fursa ambazo unajiambia zinapatikana eneo fulani, usichojua ni kwamba zinaanzia ndani yako.

Kule unakoenda kuzifuata fursa ni kutoa kile ambacho tayari kipo ndani yako.
Hivyo kabla hujazunguka kutafuta kile unachoamini umekosa, kaa kwanza chini na jitafakari kwa kina, utaweza kuona kwa urahisi jinsi ambavyo chochote unachotaka kutafuta tayari kipo ndani yako, kipo hapo ulipo.

Unewahi kujiambia huoni kitu gani cha kufanya kwa hapo ulipo, halafu akaja mtu na akaanza kufanya kitu ambacho unajiuliza mbona wewe hukuona?
Hukuona kwa sababu hukuangalia. Wewe ulikuwa unakazana kuangalia mbali na ukaacha hapo karibu.

Chochote unachofanya sasa, ndiyo chenye nguvu ya kukufikisha popote unapotaka kufika kwenye maisha yako.
Biashara uliyonayo sasa ndiyo mbegu kubwa ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Kazi uliyonayo sasa, ndiyo hatua ya wewe kufika mbali zaidi.
Badala ya kupoteza muda wako kufikiria unahitaji biashara nyingine au kazi nyingine, hebu weka juhudi hapo kwanza na ona kama hutapata matokeo ya tofauti.

Hii haimaanishi kwamba utabaki hapo milele, lakini utaanza kukua zaidi ukianzia hapo na siyo kutafuta sehemu nyingine utakayoweza kuanzia ukifikiri ndiyo sahihi zaidi.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuanzia hapo ulipo sasa.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa