Experience is one thing you can’t get for nothing. —Oscar Wilde

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UZOEFU WA BURE…
Ni rahisi sana kupata ushauri wa bure, kutoka kwa watu ambao hata hujawaomba ushauri.
Lakini huwezi kupata uzoefu wa bure.

Ushauri no rahisi kwa sababu ushauri unatolewa kwa kuongea.
Na kuongea kila mtu anaweza kufanya hivyo.
Mtu anaweza kukushauri kwa kitu alichosikia kwa wengine, na akawa na uhakika kabisa kwamba ndiyo kitu sahihi kufanya.

Lakini kwenye uzoefu siyo maneno bali matendo.
Uzoefu unayokana na kufanya.
Uzoefu unatokana na kushindwa, na ukajifunza kutokana na kushindwa huko.
Uzoefu ni kitu kimoja ambacho huwezi kukipata bure.
Itakugharimu nguvu, muda, fedha, na hata hisia zako kupata uzoefu unaotaka.

Kuna mtu anaweza kushauriwa kitu dakika moja na yeye akawa mshauri kwa wengine.
Lakini ili uwe na uzoefu wa kuweza kiwashirikisha wengine, lazima uwe umefanya kwa muda.

Kuupata uzoefu, kuwa tayari kuweka kazi, kuwa tayari kuweka muda.
Ukawe na siki bora sana ya leo, siku ya kujenga uzoefu wako zaidi na zaidi.
#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha