Siku mpya na nzuri sana kwetu.
Siku ya kipekee ambapo tumepata nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA KILA MTU ANAWEZA KUFANYA, USIFANYE…
Chochote kinachofanywa na kila mtu huwa kina thamani ndogo.
Hivyo njia bora kwako kupima ufanye nini, ni kuangalia wangapi wanaweza kufanya.
Ukifanya kile ambacho kila mtu anaweza kufanya, kwa namna ambayo wanafanya, utaishia kupata matokeo wanayopata, ambayo ni ya kawaida sana.
Njia pekee ya kupiga hatua kubwa ni kufanya kile ambacho hakuna wengi wanaoweza kufanya, au kukifanya kitu kwa namna ambayo wenye uhitaji wanakipata kwako tu.
Na hilo siyo gumu hata kidogo.
Ukiacha kuishi maigizo na ukaanza kuishi maisha ya uhalisia wako, utaona jinsi ambavyo kuna mengi unaweza kufanya tofauti.
Lakini wengi wamekuwa hawawezi kuishi uhalisia wao kwa sababu hawapendi kusemwa au kukosolewa na wengine wanaoishi kwa mazoea.
Kabla hujaanza au kuendelea kufsnya chochote unachofanya, jiulize je kila mtu anaweza kufanya kama unavyofanya? Kama jibu ni ndiyo basi kuna makosa unafanya.
Amua kuwa tofauti, chagua kufanya tofauti na hilo litakutofautisha na wengine na kukuwezesha kufanikiwa zaidi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kwenda kufanya kwa utofauti na upekee.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha