Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUWA BORA LEO ZAIDI YA JANA…
Pamoja na malengo na mipango mikubwa tunayojiwekea kwenye maisha yetu,
Pamoja na juhudi kubwa ambazo tunaendelea kuchukua kila siku kwenye maisha yetu,
Tunaweza kupiga hatua zaidi kama tutafanyia kazi msingi huu mmoja.
Kuhakikisha leo tunakuwa bora zaidi ya tulivyokuwa jana.
Tukiweza kusimamia maingi huu, hakuna chochote kinachoweza kutushinda.
Kwa sababu kama kila siku mpya tunakuwa bora zaidi kuliko siku iliyopita, maana yake tunapiga hatua zaidi.
Kwa kila siku kuwa bora zaidi ya siku iliyopita, tunajikuta tukiwashinda wengine bila hata ya kuahindana.
Kwa kila siku kupiga hatua hata kama ni ndogo, tunajikuta tumefika mbali zaid ya pale tunaponzia.
Na haijalishi utofati wa ubora wa leo na jana ni kiasi gani,
Hata kama unakuwa bora leo kwa asillimia 1 zaidi ya jana, inatosha sana, kama utafanya kila siku bila ya kuacha.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana. Siku ya kujifunza na siku ya kuchukua hatua kubwa.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha