Mpendwa rafiki,
Ukiwa na uzoefu katika eneo fulani la maisha yako huwa inalipa sana, uzoefu huwa ni kitu ambacho hakikutafuti bali wewe ndiyo unakitafuta, hakuna mtu aliyezaliwa na uzoefu wa kitu fulani. Labda tu mtoto anapozaliwa yeye bila kuwa na uzoefu lakini anajua kulia na kunyonya na vingine vyote anakuja kujifunza hapo baadaye.
Uzoefu wa kitu chochote unaongeza ufanisi wa kazi hivyo usisubiri uzoefu bali ingia na fanya utapata uzoefu. Kama unataka kuanza biashara na kisingizio kwako siyo mtaji bali ni uzoefu basi ushauri wangu kwako ni huu rafiki yangu; anza kidogo na kua na uzoefu yaani start small and grow with experience. Usitake uanze na mambo makubwa ili upate uzoefu bali anza tu na mambo madogo hayo mambo madogo ndiyo yatakuja kukupa uzoefu.
Unapoanza kidogo unapata uzoefu hivyo kadiri unavyofanya unajikuta unauzoefu. Uzoefu pekee unapatikana kwa njia ya kufanya kwa vitendo na siyo kuongea. Acha kuhubiri na ingia kaweke kazi na utafanikiwa, usilalamike sina uzoefu bali anza kufanya ndiyo utapata uzoefu kwa sababu hakuna mtu ambaye alizaliwa ni mtaalamu kabisa, wewe na mimi hatukuzaliwa tunajua kusoma lakini tumejifunza na leo tunawasiliana kwa njia ya fasihi andishi.
SOMA; Mambo Matano Muhimu Kuzingatia Ili Kuimarisha Huduma Mteja Anayopata Kwenye Biashara Yako.
Kila mtu anaweza kuwa mtaalamu na kuwa na uzoefu kama tu akiamua kuchukua hatua na kuanza kufanya kile anachokipenda. Kama unataka kuanza biashara anza, uzoefu wa biashara utaupata pale siku utakapoamua kuondoa laana na kuingia uwanjani. Hata uchukue miaka 10 kujifunza biashara kwa kusoma vitabu na kuhudhuria kama hutojifunza kwa vitendo huwezi kupata uzoefu hata siku moja.
Hatua ya kuchukua leo, vitendo ndiyo msema kweli, analipa na anakupa uzoefu hivyo weka kazi na ingia katika eneo unalotaka kuanza. Utakapoanza mfumo utakufundisha uzoefu wa biashara.
Kwahiyo, huwezi kupata kile unachokitaka kwa njia ya kuongea na kulalamika tu, bali utakipata kama ukiamua kuchukua hatua leo kama huamini hilo jaribu leo na uone matokeo.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net
Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti hii hapa www.mtaalamu.net/kessydeo .
Asante sana na karibu sana !