Siku mpya,
Siku bora,
Na siku ya kipekee sana kwetu.
Leo hii tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari INGEKUWA RAHISI KILA MTU ANGEPATA…
Kama unataka kitu ambacho wengine hawana,
Kitu kinachoitwa urahisi unapaswa kuachana nacho mara moja,
Kama unataka kufika ambapo wengine hawajafika,
Kutegemea kwamba safari hiyo itakuwa rahisi ni kujidanganya.
Wale unaoona hawajapata au kufika kule unakotaka kufika siyo wajinga sana kuliko wewe, na pia wewe siyo mjanja sana kuliko wao.
Ni kwamba ni vigumu sana kupata au kufika kwenye hatua hiyo, na wengi hawana uvumilivu na pia hawapo tayari kuweka juhudi kubwa zaidi wakati hawaoni matokeo ya haraka.
Ingekuwa rahisi kila mtu angepata anachotaka na kufika anakotaka.
Lakini siyo rahisi, ndiyo maana wengi wamekubali maisha ya ukawaida, yasiyo ya mafanikio, kwa sababu wameushindwa ugumu.
Unapochagua kupiga hatua, lazima uwe tayari kwa ugumu wowote ambao utakutana nao.
Na lazima uwe umefanya maamuzi kwamba utapata unachotaka na kufika unakotaka, au utafia njiani ukiweka juhudi za kuhakikisha unapata na kufika unakotaka.
Hayo siyo maamuzi rahisi kufanya, ndiyo maana wachache sana ndiyo wanaoweza kupata mafanikio makubwa zaidi.
Je wewe ni mmoja katika hao wachache?
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutokutafuta urahisi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha