Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA NI MWENDO….
Moja ya sifa kuu za viumbe hai ni mwendo,
Viumbe hai vyote vina sifa ya kuweza kutoka eneo moja na kwenda eneo jingine, hata kama ni taratibu au haraka.
Hata vitu visivyo hai, bado pia vina mwendo. Mawe yanakuwa kwenye mwendo na hata dunia yenyewe ipo kwenye mwendo.

Miilo yetu pia ipo kwenye mwendo.
Moyo wako upo kwenye mwendo muda wote kusukuma damu kwenda kila eneo la mwili.
Mapafu yako yapo kwenye mwendo kuingiza hewa safi na kutoa hewa chafu.
Utumbo wako upo kwenye mwendo, kumeng’enya chakula na hata kuondoa uchafu mwilini.

Bila ya mwendo, mwili wako hauwezi kuishi. Ndiyo maana kipimo rahisi cha maisha, kutaka kujua kama mtu yupo hai ni kusikiliza mapigo ya moyo na kuangalia mwendo wa upumuaji.

Sasa rafiki, mafanikio kwenye maisha pia ni matokeo ya mwendo.
Mafanikio hayatakufuata pale ulipokaa, ni lazima uwe kwenye mwendo.
Lazima uchukue hatua kila wakati ili kuweza kufanikiwa.
Na hata unapoyapata mafanikio, kama utaacha mwendo mafanikio yataondoka, na pia hutajisikia vizuri.

Hivyo rafiki, mara zote kuwa mwenye mwendo.
Na mwendo ndiyo dawa ya kujisikia vibaya, kukata tamaa na kukosa mudi.
Kama hujisikii vizuri, usikae tu, utazidi kutokujisikia vizuri, jiweke kwenye mwendo na utasahau ulikuwa unajisikiaje.
Kadhalika kwenye kukata tamaa na kukosa mudi, wewe chagua kufanya kitu, hasa kitu unachopenda kufanya, na utasahau kabisa kwamba ulikuwa unataka kukata tamaa au hukuwa na mudi nzuri.

Tiba ya kila kinachokuzuia kifanikiwa sasa hivi ni mwendo.
Kuwa na mwendo zaidi, ongeza mwendo zaidi na hutabaki hapo ulipo sasa.

Ukawe na siki bora sana ya leo, siku ya mwendo kila wakati.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha