The future belongs to those who believe in the beauty of their dreams. —Eleanor Roosevelt

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari AMINI KWENYE UZURI WA NDOTO ZAKO…
Kila mtu ana ndoto fulani kwenye maisha yake.
Hata kama mtu hasemi ndoto hiyo kwa wengine, anapokuwa peke yake, anaona mpaka taswira ya ndoto hiyo.
Anajiona akiwa kwenye mafanikio anayotaka, akiwa kwenye nafasi anayotaka kufikia.
Pia anajaribu kufanya maamuzi kama anheshakuwa kwenye nafasi hiyo.

Lakini wengi ndoto zao hubaki kuwa ndoto muda wote.
Hawathubutu kuanza kuishi ndoto zao.
Wapo wanaojaribu na wanakatishwa tamaa, au wanashindwa na wanajiambia waache utoto na badala yake wafanye vitu vya kwaida.

Kitu kinachowazuia wengi kufikia ndoto zao ni kutokuamini kwenye uzuri wa ndoto zao.
Wengi hawaamini kama kweli wanaweza kufikia ndoto hizo, hivyo hawachukui hatua wanazopaswa kuchukua.

Amini kwenye uzuri wa ndoto yako,
Amini kwamba ni maisha unayoweza kiyafikia,
Na amini kwa juhudi, uvumilivu na ung’ang’anizi utaweza kuifikia.
Na hata unapokutana na ugumu, jua ni sehemu ya safari na siyo ukomo wa safari.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuamini kwenye ndoto yako na kuchukua hatua ili kusogea karibu zaidi na ndoto hiyo.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha