Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUPOOZA KIMAAMUZI…
Ipo dhana inaitwa ANALYSIS PARALYSIS…
Hapa mtu anashindwa kufanya maamuzi na kuchukua hatua kwa sababu ya uchambuzi na upembuzi yakinifu.

Mtu anapata wazo la kufanya kitu, lakini haanzi mara moja, badala yake anaweka mipango kwanza, kitu ambacho siyo kibaya.
Ubaya unakuja pale ambapo mipango haiishi. Anapanga na kupangua, anachambua kila kitu kwa umakini.

Sasa, kadiri mtu anavyochambua kitu kwa kina, ndivyo anavyozidi kujawa na hofu na kuogopa kuanza.
Kadiri mtu anavyopanga, ndivyo anavyojiona bado hajawa tayari.
Na hapa ndipo wengi wanapofilia KUPOOZA KIMAAMUZI.
Wanakuwa na taarifa za kutosha kuhusu kitu, lakini hawawezi kufanya maamuzi.
Maana taarifa nyingi walizopata, zimezidi kuwachanganya badala ya kuwasaidia.

Kuepuka changamoto hii ya kupooza kimaamuzi, punguza muda kati ya wazo na kuchukua hatua.
Ukishapata wazo, ambalo unaamini ni sahihi kwako, anza kuchukua hatua kabla hata hujawa tayari.
Anza kwanza na utapanga baadaye.
Usipoteze muda wako kwenye uchambuzi na upembuzi unaokujaza woga zaidi ya kukupa ujasiri wa kuanza.

Kwenye shule ya matumizi ya silaha, wanatumia kanuni hii; KUWA TAYARI ➡ LENGA ➡ FYATUA.
Kwenye mafanikio kanuni inabadilika na kuwa; KUWA TAYARI ➡ FYATUA ➡ LENGA.
Huhitaji kulenga ndiyo ufyatue, hapo ndipo unakwama kwenye uchambuzi usioisha.
Unahitaji kifyatua halafu upambane na kulenga.

Ukawe na siku bora sana leo, siku ya kuepuka kupooza kimaamuzi kwa kuanza kuchukua hatua na mipango ifuate baadaye.
#Fanya#HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha