Siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KESHO HAITAKUWA TOFAUTI SANA NA LEO…
Ni rahisi sana kujiambia utafanya kesho, kile ambacho ulipanga kufanya leo.
Lakini ukweli ni kwamba, kesho haitakuwa tofauti sana na leo.
Na tena huenda kesho ikawa vigumu zaidi kufanya kuliko leo,
Kwa sababu hujui nini kitatokea hiyo kesho.
Hivyo chochote ulichopanga kufanya leo, hakikisha unakifanya leo.
Usikubali kabisa kuahirisha chochote mpaka kesho.
Usijidanganye kwamba kesho utakuwa bora zaidi, au utakuwa tayari zaidi au mambo yatakuwa mazuri.
Fanya sasa au hutafanya kabisa, maana kila wakati unakutana na mengi zaidi ya kufanya.
Kama kitu ni muhimu zaidi, kifanye leo, hata kama hutamaliza kikifanya, angalau anza kufanya.
Hii itakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kesho kuliko usipoanza kabisa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya yote uliyopanga kufanya.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha