Ni kufa.

Ikishakufa, hakuna kitu kinaweza kuwa hatari tena kwenye maisha yako, kwa sababu huna tena maisha.

Lakini kama upo hai, basi kuna hatari unatembea nazo na unapishana nazo kila siku ya maisha yako.

Kutoka tu nje ya nyumba yako ni hatari ya kutosha. Labda tumeenda mbali, kukaa ndani ya nyumba yako ni hatari. Nyumba hiyo inaweza kuvunjika na ukaumia ukiwa ndani.

Bado hapo hujatumia vyombo vya usafiri ambavyo vina hatari ya kupata ajali, hujatumia vifaa mbalimbali vinavyoweza kukuumiza, hujakutana na watu ambao wanaweza kukudhuru.

Ninachotaka kukuambia hapa rafiki yangu, achana na kuangalia hatari, na badala yake angalia umuhimu wa chochote unachotaka kufanya.

Kwa mfano, kama mtu anasafiri na gari, kisha gari ikapata ajali akiwa njiani, akaumia, je atasema sipandi tena gari namalizia safari yangu kwa kutembea? Hapana, mtu anatoka kwenye ajali ya gari na kupanda gari nyingine, hapo hapo, bila hata ya kufikiria mara mbili.

Sasa kwa nini mtu huyo huyo, anapoanzisha biashara ikapata hasara au kufa anajiambia hatafanya tena biashara? Kwa nini mtu huyo huyo anapoingia kwenye mahusiano na mtu mmoja na hayakuenda vizuri anaona mahusiano hayafai kabisa?

Nafikiri unaona jinsi gani hatari nyingi tunazokwepa, hatuangalii umuhimu wake au hatupo tayari kuweka kazi tunayopaswa kuweka.

Kama kitu ni muhimu kwako, utakifanya, bila ya kujali kiasi cha hatari kilichopo kwenye kitu hicho.

Hivyo nikukumbushe tena rafiki, njia pekee ya kuivuka hatari, ni kuikabili. Usikimbie hatari, usijifiche, bali ikabili, ukiwa umejitoa kukabiliana na kila utakachokutana nacho.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha