Nimekutana na dhana hii ambayo nimeona ni nzuri sana kuijaribu kwenye biashara.

Kama una biashara ambayo unahitaji kutangaza ili kuwafikia wengi, badala ya kutumia fedha kwenye matangazo, tumia fedha hiyo kwenye bidhaa au huduma ambazo unatoa kwa watu.

Yaani ukishajua kiasi cha fedha unayopaswa kulipa kwenye matangazo ni kiasi gani, chukua thamani ya bidhaa au huduma na toa bure kwa wateja ambao wanaweza kuitangaza vizuri zaidi biashara yako.

Na hii itakuwa njia nzuri sana ya bidhaa au huduma yako kuwafikia wengi.

Badala ya kupoteza fedha nyingi kwenye matangazo ambayo hayawafikii walengwa, ni bora kutumia gharama hizo kuwafikia walengwa moja kwa moja.

Naona hii ni njia bora sana ya kutumia bajeti yako ya matangazo. Toa bidhaa au huduma yako kwa watu ambao wanaweza kuwafikia wengi zaidi.

Na makampuni makubwa yameanza kutumia njia hii, hasa kwenye zama hizi za mitandao ya kijamii. Kampuni inampa mtu kitu cha bure, lakini inabidi awe anaonesha kwenye mitandao ili wengine waone na kuwa wateja.

Unaweza kuangalia ni kwa namna gani bidhaa au huduma unayouza, unaweza kuwachagua watu fulani wakapata bidhaa au huduma ya bure, na wakawa mabalozi wazuri wa biashara yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha