“Hang in there no matter what. While there are probably a number of things in your life that would be convenient to quit on, your success is definitely not one of them. Stick and stay. It’s bound to pay.” – Grant Cardon
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Siku ya leo, sisi tunapata nafasi nzuri ya kwenda kuweka kuhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Tunaianza siku hii tukiwa na matumaini kwamba tutaweza kupiga hatua kubwa kwa juhudi tunazokwenda kuweka, na pia tutajifunza mengi.
Tutaimaliza siku ya leo, tukiwa bora kuliko tulivyoianza.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio, tunaouishi kila siku bila ya kuuvunja ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kuishi msingi huu leo na utatuwezesha kupiga hatua kubwa.
Pia mwaka huu 2018 tunaongozwa na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo leo tutatatua matatizo makubwa na magumu, tutafanya maamuzi magumu na kuwa mfano kwa kila tunachofanya.
Asubuhi ya leo tutafakari MAFANIKIO NI KUKOMAA…
Najua unajua hili, lakini nisipolukumbusha mara kwa mara utaanza kujidanganya, hasa pale utakapoanza kuwasikiliza wanaokuambia kuna njia za mkato za kufanikiwa. Watakushawishi kweli na utajiambia kwani kuna ubaya gani nikijaribu? Unajaribu na hapo unapotea moja kwa moja.
Mafanikio ni kukomaa rafiki,
Njia haitakuwa rahisi,
Utakuwa na kila sababu ya kukata tamaa na kuacha.
Lakini kitu pekee ambacho hupaswi kukikatia tamaa kwenye maisha yako ni mafanikio yako.
Mafanikio yako ni jukumu lako la kwanza kwenye maisha, hivyo ukikata tamaa kwenye hilo, huna hata haja ya kuendelea kuwa hai.
Pambana, komaa, vumilia, ng’ang’ana mpaka upate kile unachotaka, licha ya ugumu wowote utakaokutana nao.
Kata tamaa kwenye mengine mengi, lakini siyo kwa mafanikio yako.
Nakutakia siku njema sana ya leo, siku ya kupambana bila ya kukata tamaa.
#Fanya#HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha