Ni rahisi sana kudanganya kwa maneno, ni vigumu mno kudanganya kwa vitendo.

Hivyo kama unataka kuujua ukweli, usisikilize watu wanasema nini, bali angalia watu wanafanya nini.

Ushahidi huwa unaongea wenyewe hata kama umechelewa.

Tumia hili kwa pande mbili.

Upande wa kwanza, pale unapotaka kujua ukweli kuhusu wengine, angalia zaidi wamefanya na wanafanya nini kuliko kile wanachosema. Unachoona kwenye tabia halisi ya mtu ni ukweli kuliko kile anachokuambia. Na pia usijidanganye juu ya tabia za watu, kwa sababu tabia hazidanganyi.

Upande wa pili, unapotaka kuwashawishi watu, acha vitendo vifanye kazi zaidi ya maneno. Usitumie maneno mengi, bali onesha nini umefanya au nini unaweza kufanya. Matendo yanasema kwa sauti kuliko maneno.

Mwisho kabisa, hakikisha unajijengea tabia zinazoendana na yale unayosema, hata kama unafikiri hakuna anayeona tabia zako, au watu wataamini unachosema, ipo siku ushahidi utakuwa wazi, na utaongea wenyewe, na kwa sauti kubwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha