Mpendwa rafiki yangu,

Maisha ni magumu tayari lakini kuna watu kadiri ya sababu zao wanayafanya maisha kuwa magumu zaidi. Mitazamo yetu juu ya mambo ndiyo inaweza kufanya maisha kuonekana kama ni magumu sana au marahisi sana. maisha ni mitazamo yetu sisi, hata pale mtu anapokutukana ukipotezea na kusema hakuna kitu wala hutoumia ila pale unapoanza kuchukulia kuwa huyu ndugu kanitukana na kujipa tafsiri za kila aina hapo hizo tafsiri unazojipa juu ya lile tusi ndiyo hupelekea wewe kuumia.

Arthur Rubinster anasema kuwa amegundua kuwa; kama ukiyapenda maisha, maisha nayo yatakupenda. Kumbe basi, changamoto kubwa inayofanya watu kuyaona maisha ni magumu sana kwa sababu hawayapendi maisha, ukiyachukia maisha nayo maisha yatakuchukia vivyo hivyo ukiyapenda maisha nayo maisha utashangaa yanakupenda.

cropped-mimi-ni-mshindi

Ndivyo ilivyo hata katika kazi zetu, wale wanaopenda kazi zao utashangaa kazi nazo zinawapenda hivyo wanajikuta wanafanikiwa kwa kutoa thamani kubwa. Natumaini unaelewa pale unapokuwa na upenzi na kitu, hivyo ile nguvu ya upenzi inakuwa inakusukuma wewe kuendelea kufanya yale yaliyo bora kabisa.

Tunatakiwa tupende kuanzia kazi tunazofanya na tunayapende maisha baada ya hapo vyote hivyo navyo vitatupenda vyenyewe. Yachukulie maisha yako katika mtazamo chanya na siyo hasi, yanaone maisha yako ni bora sana kuliko mtu mwingine na usijifananishe na mwingine kwani unapojifananisha utakosa upekee wako si unajua wewe ni mtu wa pekee hapa duniani una kitu ambacho mtu mwingine hana.

SOMA; Hii Ndiyo Njia Pekee Ya Kukuwezesha Wewe Kufanya Kazi Zaidi Ya Wengine Na Kufanikiwa Zaidi.

Ukikutana na watu wanaongea mabaya juu ya maisha usiwape nafasi ya kuwasikiliza hata kidogo, wale wanaolalamika kuwa maisha ni magumu usiwape nafasi kabisa ya kusikiliza nyimbo zao za kila siku, wape nafasi watu ambao wana vitu chanya wanaweza kukusaidia au mkasaidiana kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Hatua ya kuchukua leo; yapende maisha yako na maisha yatakupenda pia. Penda kazi yako au kile unachofanya utapata matokeo mazuri sana.

Hivyo basi, tunapata kile ambacho tunakifikiria kwenye maisha yetu kadiri ya mitazamo yetu hivyo kuwa na mtazamo sahihi siku zote ili uweze kuvutia vitu chanya kwenye maisha yako.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !